Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 27/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 27/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 27/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Odinga azindua harakati za kutafuta haki baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu

media Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Reuters/Noor Khamis

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema hawezi kukubali wito wa kuyakubali matokeo ya urais baada ya Uchaguzi Mkuu wiki mbili zilizopita, yaliyompa ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza mjini Mombasa, alikohudhuria sherehe za kumwapisha Gavana wa Mombada Hassan Joho, Odinga amesema hatarudi nyuma katika shinikizo za kutaka ukweli kufahamu kuhusu matokeo ya Uchaguzi wa urais.

Aidha, amesema kuwa muungano wa NASA umezindua kampeni ya kufahamu ukweli wa kilichojiri wakati wa Uchaguzi Mkuu, na kudai haki kuhusu Uchaguzi.

“Hatutakubali na kusonga mbele kama tunavyoambiwa, hatutakubali, hatutakubali wizi wa kura,” alisema Odinga huku akishangiliwa na wafuasi wake.

Odinga amesema historia ya siasa nchini Kenya inaonesha wazi kuwa, haki nchini Kenya haijawahi kupatikana kupitia Mahakama au bunge, bali kupitia wananchi wenyewe  kuchukua hatua.

“Huu ni wakati wa vijana kuamka na kukataa wizi wa kura, lazima tupinge hili lote na kusimama pamoja,” aliongeza Odinga.

Kiongozi huyo wa NASA, ametoa kauli hii wakati huu Mahakama ya Juu inapojiandaa kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.

Upinzani umewasilisha ushahidi wenye kurasa zaidi ya 20,000 kutaka Mahakama kubadilisha matokeo na kutaka Uchaguzi mwingine kufanyika.

Kenyatta katika hatua nyingine, amekuwa akihimiza amani na kuwataka Wakenya kusonga mbele baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana