Pata taarifa kuu
RWANDA

Rais Kagame aapishwa kuongoza Rwanda kwa muhula wa tatu

Paul Kagame ameapishwa kuongoza nchi ya Rwanda kwa muhula wa tatu, katika sherehe za kufana zilizofanyika siku ya Ijumaa katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame  wakati akisaini kiapo baada ya kuapishwa Ijumaa, Agosti 18 2017
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakati akisaini kiapo baada ya kuapishwa Ijumaa, Agosti 18 2017 Paul Kagame Twitter
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya raia wa Rwanda walifurika kuja kushuhudia kuapishwa kwa Kagame ambaye amepata nafasi nyingine ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka saba, baada ya kuingia madarakani mwaka 2000.

Mbali na wananchi, wanajeshi walipamba sherehe hizo ambazo pia zilihudhuhuriwa na marais zaidi ya 10 kutoka barani Afrika ,wakiwemo  Mabalozi wa nchi mbalimbali.

Kagame ameahidi kuilinda na kuiheshimu katiba ya Rwanda na kuwafanyia kazi raia wa nchi hiyo na kuwasaidia kuinua uchumi wao.

Aidha, amesema pamoja na wale wanaompinga, na wanaisihi nje ya nchi, wawe tayari kufanya kazi ya kuisaidia nchi yao.

Raia wa Rwanda wamesema wana imani kubwa kuwa kiongozi wao atasaidia kutatua changamoto zinazowakabili hasa ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kuapishwa kwa Kagame kumekuja baada ya kupata ushindi wa asilimia 98.7 baada ya kuwapiku wapinzani wake Frank Habineza na Philippe Mpayimana.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.