Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Raila Odinga : Niko tayari kufichua wizi wa kura

media Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga. REUTERS/Thomas Mukoya

Wakati ambapo hali ya utulivu ikianza kurejea nchini Kenya, kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akihojiwa na gazeti la Financial Times la Uingereza amesema kwamba atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura.

Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.

“Niko tayari kuonyesha jamii ya kimataifa na Wakenya jinsi gani tulivyoibiwa kura zetu, “ amesema Bwa Odinga .

Raila Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne alishindwa katika uchaguzi huo wa urais uliyofanyika Agosti 8, 2017. Pia alibaini kwamba hatowania tena urais , huku akisema aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.

“Natangazia Wakenya kwamba sitawania tena urais. Tumependelea tu Wakenya kujua mchezo uliopigwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017. Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, “ ameongeza Raila Odinga.

Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi imefutilia mbali madai hayo ikibaini kwamba ni madai yasiokuwa na msingi.

Machafuko ya hivi karibuni nchini Kenya yamesababisha vifo kadhaa na watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kukamatwa.

Vikosi vya usalama katika eneo la Kibera mjini Nairobi, ambapo mvutano na makabiliano vilishuhudiwa siku ya Jumamosi, Agosti 12, 2017. MARCO LONGARI / AFP

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana