Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wafuasi wa Odinga waandamana jijini Nairobi na Kisumu

media Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi mtaani Mathare jijini Nairobi www.reuters.com

Hali ya wasiwasi inaendelea kushuhudiwa katika mitaa kadhaa ya jiji kuu la Nairobi na Kisumu nchini Kenya baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa Uchaguzi wa urais Ijumaa usiku.

Maandamano ya wafuasi wa muungano wa upinzani NASA, yamekuwa yakiendelea usiku kucha dhidi ya polisi, kulalamikia madai ya mgombea wao Raila Odinga kuibiwa kura.

Mjini Kisumu Magharibi mwa nchi hiyo, ambayo pia ni ngome kuu ya Odinga, wafuasi wake wameendelea kuandamana kupinga ushindi wa Kenyatta.

Wafuasi wa Odinga walioonekana wenye hasira, wamenukuliwa na runinga ya KTN nchini humo wakisema hawayakubali matokeo hayo.

“Kama hamna Raila Odinga, hakuna amani,” alisema mmoja wa waandamanaji.

“Inakuwaje Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alituambia tupuuze matokeo tuliyokuwa tunayaona kwenye runinga na wakaamua kutatangaza ?,” alihoji mwandamanaji mwingine kwa hasira.

Mwandishi wa Habari wa kituo cha KTN Duncan Khaemba alikamatwa na Polisi akiripoti kinachoendelea huku wengine wakizuiwa kufika mtaa wa Kibera.

Waziriwa usalama Fred Matiang'i naye amejitokeza na kukanusha madai kuwa Polisi wanawapiga risasi waandamanaji.

Matiang'i ameongeza kuwa, wanaoandamana wanajihusisha na wizi na uharibifu wa mali na hivyo si waandamanaji bali wameamua kutumia hali hii ya wasiwasi kufanya wizi.

“Sina taarifa zozote za mtu yeyote aliyepigwa mbaye amepigwrisasi na polisi hapa nchini, polisi hawajatumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, “ amesema.

“Hili naweza kukuambia wazi na kukiri kuwa ni uongo kwa sababu inatoa utaratibu wa Polisi kuwalinda waandamanaji,” ameongeza.

Waandamanaji mtaani Mathare jijini Nairobi Photo: AFP/Tony Karumba

Ripoti zinasema kuwa baada ya makabiliano ya usiku kucha kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama hasa katika mtaa wa Kondele, watu wawili wamepigwa risasi na kuuawa huku wengine wakijeruhiwa kwa mujibu wa Daktari Ojwang Lusi, mjini Kisumu.

Mwakilishi wa serikali katika eneo hilo Wilson Njenga hata hivyo amesema kuwa mtu mmoja ndiye aliyeuawa katika eneo la Maseno baada ya kupigwa risasi akijaribu kufanya wizi.

Aidha, amekanusha madai ya polisi kuwa mtaani na kuwalazimisha wafuasi wa upinzani kutoka ndani ya nyumba zao na kuwapiga risasi.

"Huu ni uongo, hakuna polisi mtaani na hakuna mtu anayetolewa ndani ya nyumba yake, kinachoendelea ni polisi kuondoa vizuizi vilivyowekwa barabarani na waandamanaji," ameongeza Njenga.

Hali ilivyo katika mji wa Kisumu, Jumamosi Agosti 12 2017 Marion Mwange/RFI Kiswahili correspodent in Kisumu

Hali hiyo pia imeshuhudiwa mjini Siaya ambapo mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na kupoteza maisha usiku wa kuamki leo.

Mtaani Kibera na Mathare jijini Nairobi, wafuasi wa Odinga wamekuwa wakichoma matairi na kufunga barabara kadhaa kuonesha hasira zao.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini humo, limelaani hatua ya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji na kuitaka kujiepusha kukabiliana na waandamanaji.

Aidha, wametoa wito kwa muungano wa NASA kwenda Mahakamani, kupinga ushindi wa rais Kenyatta.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana