Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-RAILA ODINGA

Raila Odinga mwanasiasa aliyekaribia sana Ikulu bila mafanikio

Raila Odinga amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya kati ya mwaka 2008-2013  na kiongozi wa siku nyingi wa upinzani, lakini matokeo ya Ijumaa usiku yameanza kumweka katika njia panda ya kutimiza azma ya kuwa rais wa Kenya.

Raila Odinga, katika mikutano yake iliyopita
Raila Odinga, katika mikutano yake iliyopita Photo: AFP/Kevin Midigo
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wake wanasema anaendelea kuwa rais bora ambaye, hakupata nafasi ya kuiongoza Kenya.

Odinga mwenye umri wa miaka 72, amewania urais kwa mara ya kwanza mwaka 1997, 2007, 2013 na sasa 2017 bila mafanikio.

Nyakati hizo zote, Odinga amekuwa akisema amepoteza mara moja tu, mwaka 1997 lakini ameibiwa katika miaka yote iliyopita. Mwaka 2007, hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya kutokea kwa machafuko ya kisiasa na kusabisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema baada ya kuanza siasa miaka ya 1980, kufungwa jela kwa muda mrefu kwa sababu ya kupinga serikali ya rais mustaafu Daniel Moi, Odinga ameendelea kuonekana kama kioo cha demokrasia nchini humo.

Kuelekea Uchaguzi wa mwaka huu, Raila alijita kama Joshua kama kiongozi aliyekuwa na nia ya kuleta mabadiliko ya uongozi na kuongoza kwa muhula mmoja tu na kuchia madaraka kwa wanasiasa wenzake katika muungano wa NASA.

Odinga alizaliwa katika Familia ya kisiasa, baba yake Jaramogi Oginga Odinga aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Kenya baada ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1963.

Aliingia bungeni mwaka 1992 wakati wa uongozi wa Moi na kuongoza harakati za muda mrefu kupambana na uongozi wa chama kimoja cha KANU.

Odinga, ambaye wafuasi wake wanamwita Baba, Agwambo, Tinga na Jakom ( Mwenyekiti) amekuwa akisema yeye ni mwanasiasa anayetaka kuona usawa nchini Kenya lakini, kukumbukwa kama mtu aliyepigania demokrasia, usawa na haki za binadamu.

Hata hivyo, wakosoaji  wake wanasema amejikita katika siasa za kuwatenganisha Wakenya lakini pia amekuwa kiongozi wa kisiasa nchini humo kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwa na rekodi yeyote ya maendeleo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.