Pata taarifa kuu
KENYA-KISUMU-UCHAGUZI

Wakenya watakiwa kudumisha amani na utulivu

Wakati ambapo taifa la Kenya likisubiri tume ya IEBC kutangaza mshindi wa urais Wakenya wamehimizwa kudumisha amani na umoja ili taifa liendelee na shughuli za kiuchumi na maendeleo.

Kisumu, wapiga kura wakipiga kura mapema asubuhi Jumanne Agosti 8, 2017.
Kisumu, wapiga kura wakipiga kura mapema asubuhi Jumanne Agosti 8, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka eneo la Kisumu sasa imetoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo kurejelea biashara zao huku mji huo ukisalia bila shughuli nyingi kama ilivyo kawaida.

Jumuiya hiyo ikiongozwa na Isreal Agina wameitaka Tume ya Uchaguzi (IEBC) kuharakisha zoezi la kuhesabu kura huku ikiarifu kuwa swala hilo linaathiri shughuli za kawaida hasa biashara na kuongezea kuwa linachangia pakubwa kuzorota kwa uchumi wa nchi ya Kenya.

Mwenyekiti wa baraza kuu la Wahubiri na Maimamu wa dini ya kiislamu nchini Shekh Abdalla Ateka vile vile amewataka wakenya kuzingatia utulivu na amani hata baada ya tume ya IEBC kutangaza mshindi wa urais.

Wagombea mbalimbali pia wametakiwa kukubali matokeo na wale ambao hawataridhishwa na matokeo hayo wafuate sheria bila ya kuchochea wafwasi wao kuvuruga Amani.

Hali ya amani na utulivu inaendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Nakuru, huku Wakenya wakisubiri Tume ya Uchaguzi nchini humo kutoa tangazo rasmi la matokeo ya uchaguzi wa urais, kwa mujibu wa mwandishi wetu Paul Silva Muchesi.

Mji wa Nakuru uko takriban kilomita 170 kutoka mji wa Nairobi, na ni mji ambao Wakenya kutoka tabaka mbalimbali wanaishi. Mji huu unaaminika kuwa ngome ya chama cha Jubilee na hilo limethibitishwa na matokeo ya awali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya Jumanne.

Hata hivyo wakazi wa mji huu wanaendelea kusubiria matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais, hali ya amani na utulivu inaendelea kushuhudiwa, huku wananchi wakipongeza tume ya uchaguzi IEBC.

Katika sehemu mbalimbali maduka hayajafunguliwa, huku wafanyabiashara wakiamua kusubiri kwanza kutangazwa kwa matokeo hayo.

Kaunti ya Nakuru, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyokua yakiendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi imempa rais uhuru kenyatta kura 631,920, huku Raila Odinga akijizolea kura 110,332 katika kaunti hii

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.