Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI MKUU 2017

UCHAGUZI KENYA 2017: Viongozi wa dini watoa wito wa amani kwa raia wa Kenya

Waumini wa madhehebu mbalimbalik ya Kikristo nchini Kenya hii leo walifurika kwa wingi kwenye nyumba za ibada, kuhudhuri misa ya mwisho ya siku ya Jumapili kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne ya wiki ijayo.

Kasisi wa kanisa Angikana la Watakatifu wote la jijini Nairobi, Sammy Wainaina. 6 Agosti 2017, Nairobi, Kenya
Kasisi wa kanisa Angikana la Watakatifu wote la jijini Nairobi, Sammy Wainaina. 6 Agosti 2017, Nairobi, Kenya Emmanuel Makundi/RFIKIswahili
Matangazo ya kibiashara

RFI Kiswahili imeshuhudia mamia kwa maelfu ya waumini wakihudhuria ibada kwenye makanisa mbalimbali, huku wengi wakisema wameenda kwaajili ya kuombea amani ya taifa lao kuelekea uchaguzi mkuu.

Katika kanisa la All Saint's Cathedral la jijini Nairobi nchini Kenya, waumini walikusanyika na kufanya sala ya pamoja kuombea taifa na kuombea uchaguzi uchaguzi mkuu.

03:12

Wakenya Wafanya Ibada Kuombea Taifa Ripoti Kamili Kutoka Kenya

Kasisi mkuu wa kanisa hili Sammy Wainaina amewataka waumini kuendelea kufanya maombi kuliombea taifa, huku akiwataka vijana kutotumiwa na wanasiasa siku ya kupiga kura.

Kasisi Wainaina amesema anasikitishwa na namna ambavyo wanasiasa walishindwa kuonesha mshikamano katika kuhubiri amani ambapo badala yake walikuwa wakifanya siasa za kuwagawa raia wa Kenya kwa misingi ya ukabila.

Wainaina amewataka wananchi na hasa vijana kujiepusha na vurugu ambapo akasisitiza kuwa taifa la Kenya linaongozwa kwa misingi ya sheria na kwamba hakutakuwa na haja kwa raia kubaki kwenye vituo vya kupiga kura kwa lengo la kulinda kura zao.

Waumini wa kanisa Anglikana All Saint's Cathedral wakifanya ibada Nairobi, 6 Agosti 2017
Waumini wa kanisa Anglikana All Saint's Cathedral wakifanya ibada Nairobi, 6 Agosti 2017 Emmanuel Makundi/RFIKIswahili

Wainaina amesema "Unajua wanasiasa wangependa kuchukua fursa yoyote kupata kura, kwa hivyo wangetumia njia zozote, mbinu zozote za kikabila za kugawanya watu na kutoa matamshi ambayo sio mazuri."

Ameongeza kuwa "Sisi kama viongozi wa kanisa tunasikitika tunaposikia hasa viongozi wakubwa wa Serikali na hata walio kwenye upinzani kutumia nafasi zao kuleta rabsha kuleta migawanyiko kwa wananchi, kwa hakika wamefanya nchi igawanyike zaidi kwahivyo ningekubaliana kwamba hawajafanya ya kutosha". alisema Kasisi Wainaina.

Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema wao wako tayari wanajiandaa kwa uchaguzi siku ya Jumanne na kwamba wana imani kubwa utakuwa huru na haki, huku wakiwataka wanasiasa watakaoshindwa kukubali matokeo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.