Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC-USALAMA

UNSC: Hali mbaya ya kisiasa yaendelea Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa ripoti ambapo linaeleza hali mbaya ya kisiasa inaendelea kushuhudiwa nchini Burundi. Baraza hilo la Usalama limeelezea kusikitishwa na hali hiyo ikiwa ni pamoja na taarifa za ongezeko la idadi ya wakimbizi, mateso, mauaji ya kinyama na kutoweka kwa watu kadhaa.

Rais wa Burundi Burundi Pierre Nkurunziza, ambaye serikali yake inalaumiwa kuendelea kupinga kuketi kwenye meza ya mazungumzu na upinzani wenye msimamo mkali (CNARED.)
Rais wa Burundi Burundi Pierre Nkurunziza, ambaye serikali yake inalaumiwa kuendelea kupinga kuketi kwenye meza ya mazungumzu na upinzani wenye msimamo mkali (CNARED.) AFP/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Burundi na pande zote zinazohusika katika visa hivyo kusitisha mara moja na kukataa matukio hayo ya vurugu kuendelea.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema linatarajia kuchukua hatua kwa wote wanaohusika na matukio hayo ndani na nje ya nchi hiyo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema hali hiyo inatishia amani na usalama wa Burundi.

Katika taarifa hiyo iliyosomwa na Balozi Amr Abdellatif Aboulatta kutoka Misri ambaye ndio mwenyekiti wa Baraza hilo, amesema Baraza hilo linasikitishwa na hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Burundi ambapo zaidi ya wakimbizi laki mbili wamekuwa wa ndani, huku watu raia milioni tatu wakiwa na mahitaji na zaidi ya raia laki nne wakitafuta ukimbizi katika nchi za jirani.

Kwa upande mwingine Baraza hilo limelaani vikali matamko katika umma ambayo yamekuwa yakihamasisha vurugu na chuki dhidi ya raia ikiwemo wito wa kulazimisha kuwapa ujauzito wanawake na wasichana na kuitaka serikali na pande zote kusitisha mara moja vurugu na kulaani kauli zote za chuki.

Baraza hilo limekaribisha jitihada za nchi zinazoendelea kupokea wakimbizi kutoka Burundi, hasa kwa kuheshimu wajibu wao wa kimataifa katika kujali hadhi za wakimbizi na kuhakikisha wanarejea walikotoka kwa hiari yao kwa kuzingatia uamuzi wao na taarifa za usalama na utu wa binadamu.

Mpaka sasa serikali ya Burundi haijaeleza lolote kuhusu ripoti hii.

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadam, na maelfu wengine kukimbilia nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.