Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Mvutano waendelea kushuhudiwa nchini Kenya siku chache kabla ya uchaguzi

Kampeni nchini Kenya zinaingia katika dakika za lala salama. kuelekea siku ya upigaji kura siku ya Jumanne wiki ijayo. Wapiga kura Milioni 19 watawachagua rais, Magavana, Maseneta, wawakilishi wa wanawake, wabunge na wawakilishi wa bunge za Kaunti.

Mwananchi akipiga kura kwenye uchaguzi uliopita nchini Kenya
Mwananchi akipiga kura kwenye uchaguzi uliopita nchini Kenya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wito wa amani umeendelea kutolewa kwa wananchi wa taifa hilo ili kuepusha machafuko yaliyozuka baada ya mwaka 2007.

Wakati huo huo muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umeitaka tume ya uchaguzi kumwajiri mtaalam mpya wa kimataifa kutoka nje ya nchi kushughulikia idara ya teknolojia lakini pia kuitaka serikali kuruhusu shirika la Ujasusi la Marekani FBI, lile la Scotland na Yark kutoka Uingereza kusaidia kuchunguza waliomuua meneja wa teknolojia katika tume hiyo ya uchaguzi Chris Msando.

Haya yanajiri wakati mamia ya wanaharakati wa kutetea haki zabinadamu waliandamana siku ya Jumanne jijini Nairobi kulaani mauaji ya meneja huyo wa Teknolojia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.