Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Rais Kenyatta akanusha madai ya kukutana na jeshi kupanga wizi wa kura

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekanusha madai ya mgombea Mkuu wa urais kupitia muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kuwa amekuwa akikutana na jeshi kupanga wizi wa kura wakati wa Uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi wa Agosti.

Rais  Uhuru Kenyatta (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi  Samson Mwathethe
Rais Uhuru Kenyatta (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi Samson Mwathethe REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta amesema madai hayo ni ya uongo na hayana ukweli wowote, na kwamba jeshi la nchi hiyo halijawahi kuingilia siasa za taifa hilo la Afrika Mashariki.

Aidha, amesema kuwa madai hayo hayana msingi wowote, na ni njama ya Odinga kutaka Uchaguzi huo kutofanyika.

Siku ya Ijumaa, Odinga akiwa na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka jijini Nairobi, walitoa nyaraka kwa wanahabari kueleza namna serikali ilivyokuwa inatumia jeshi kuingilia Uchaguzi huo.

Odinga alidai kuwa, tayari kuna karatasi bandia za kupigia kura za  urais, ambazo amesema zitatumiwa kumwongezea rais Kenyatta kura katika ngome zake na tayari zimeshaingia nchini.

Msemaji wa jeshi nchini humo Joseph Owuoth amethibitisha kuwa nyaraka zilizotolewa na Odinga ni za kweli, lakini zinahusu oparesheni ya Dumisha utulivu, kipindi cha Uchaguzi wala sio kuiba kura.

Owuoth ameongeza kuwa  kuwa jeshi nchini humo lakini maslahi yoyote na katika Uchaguzi na siasa za nchi hiyo, na linasalia kutoegemea upande wowote.

Yote haya yanakuja siku chake kuelekea Uchaguzi huo huku ushindani mkubwa wa kiti cha urais ukiwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga licha ya kuwa na wagombea wengine sita.

Tume ya Uchaguzi inasema, iko tayari kuandaa Uchaguzi huo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.