Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA

Tanzania yakanusha madai ya kuingilia siasa za Kenya

Serikali ya Tanzania imekanusha madai kuwa inaingilia siasa za Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi ujao.

Waziri wa Mambi ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga
Waziri wa Mambi ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Augustine Mahiga, amesema nchi hiyo haina uwezo wa kuingilia Uchaguzi wa nchi jirani.

Aidha, ameongeza kuwa, Tanzania inaheshimu uhuru wa nchi ya Kenya na haina teknolojia yoyote ya kushawishi matokeo ya Uchaguzi wa urais.

Mahiga ametoa kauli hii baada ya madai katika vyombo vya Habari nchini Kenya kuwa, muungano wa upinzani NASA umeandaa kituo cha kujumuishia matokeo nchini Tanzania.

Waziri huyo ameongeza kuwa, Tanzania inaheshimu na inaamini katika demokrasia na haiwezi kuingilia siasa au Uchaguzi wa nchi nyingine.

Serikali ya rais Uhuru Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili, imeonekana kuwa na wasiwasi kuhusu madai hayo na inaaminiwa kuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Amina Mohammed amelizungumzia katika ziara yake nchini Tanzania.

Raila Odinga atakayeperusha bendera ya muungano wa NASA, amekuwa akisema, muungano huo utakuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo lakini haijafamika eneo la kituo hicho.

Rais John Magufuli ambaye ni rafiki wa Odinga, amejiweka kando na siasa za Kenya na hajasikika akisema lolote au kuonesha anaegemea upande gani.

Hata hivyo, chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kimetangaza wazi kuwa kinaunga mkono kuchaguliwa kwa Odinga.

Naye aliyekuwa mgombea wa urais mwaka 2015 Edward Lowassa na chama kikuu cha CHADEMA, kimesema kinaunga mkono kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.