Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Muungano wa NASA washindwa katika kesi nyingine dhidi ya IEBC

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umepoteza kesi nyingine dhidi ya Tume ya Uchaguzi IEBC baada ya ile uchapishaji wa karatasi za kupigia kura siku ya Alhamisi.

Jengo la Mahakama Kuu jijini Nairobi
Jengo la Mahakama Kuu jijini Nairobi Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

NASA ambayo imesema itakwenda katika Mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, ilikwenda Mahakamani kuitaka Tume hiyo kutumua mfumo wa kieletroniki kama njia mbadala ya kuwatambua wapiga kura ikiwa mfumo uliopo utagoma.

Aidha, upinzani ulitaka Mahakama kuamua kuwa ikiwa mfumo huo hautafanya kazi uchaguzi uahirishwe katika maeneo yatakayoathiriwa.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi imekuwa ikijitetea kuwa mfumo mbadala wa kuwatambua wapiga kura kupitia daftari la kupigia unaweza kutumiwa ikiwa mfumo wa eletroniki utakwama.

Wapinzani wamekuwa wakisema kuwa mfumo pekee unaoweza kuzuia wizi wa kura ni mfumo wa kieletroniki.

Majaji Kanyi Kimondo, Hedwig Ong’udi na Alfred Mabeya kwa pamoja wamesema wameridhishwa na maelezo ya IEBC kuwa mfumo huo mbadala utasaidia kuwatambua wapiga kura ikiwa mitambo ya eletroniki itagoma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.