Pata taarifa kuu
TANZANIA-UPINZANI

Mawakili wazuiwa kuonana na mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu

Mawakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu aliyekamatwa siku ya Alhamisi katika uwanja wa ndege jijini Dar es salaam, wanasema hawajaruhusiwa kumwona na kuzungumza na mteja wao.

Tundu Lissu, mbunge wa upinzani nchini Tanzania na rais wa chama cha Mawakili nchini humo (LST) anayezuiliwa na polisi.
Tundu Lissu, mbunge wa upinzani nchini Tanzania na rais wa chama cha Mawakili nchini humo (LST) anayezuiliwa na polisi. Yutube
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa Wakili wa Lisu, Fatma Karume ameliambia Gazeti la Mwananchi kuwa, hajaruhusiwa kumwona mwanasheria huyo wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA lakini pia rais wa chama cha Mawakili nchini humo, licha ya kufika katika makao makuu ya Polisi tangu asubuhi.

Aidha amesema kuwa Polisi wamemwambia kuwa mwanasiasa huyo hawezi kupewa dhamana siku ya Ijumaa,  kwa sababu uchunguzi dhidi yake haujakamilika.

Hakuna sababu zilizotolewa na Polisi kuhusu kukamatwa kwa mwanasaisa huyo ambaye pia ni mbunge.

Hivi karibuni, alinukuliwa na vyombo vya Habari kwa kumwita rais John Magufuli kama dikteta yeye pamoja na serikali yake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Lissu kukamatwa na kuzuiwa na Polisi kwa kumwita rais Magufuli, dikteta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.