Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Rais Pierre Nkurunziza afanya ziara nje ya nchi kwa mara ya kwanza tangu 2015

media Rais wa Burundi Piere Nkurunziza alivyokaribishwa na rais wa Tanzania John Magufuli Julai 20 2017 wilayani Ngara Ikiriho

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameondoka nchini mwake kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka miwili, tangu kutofanikiwa katika  jaribio la kumwondoa madarakani mwaka 2015.

Nkurunziza amezuru nchini Tanzania katika Wilaya ya Ngara, kukutana na mwenyeji wake rais John Magufuli.

Ziara hii imekuja wakati huu Tanzania ikiendelea kutoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 200,000 waliokimbia nchi yao kwa sababu za kiusalama.

Rais Nkurunziza ameandamana na idadi kubwa ya Mawaziri wake katika ziara hiyo ya kwanza ambayo ilitangazwa katika dakika za lala salama.

Jaribio la kumpindua Nkurunziza lilifanyika wakati akihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiwahotubia wananchi, rais Nkurunziza amewaambia wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania kurejea nyumbani ili kuijenga nchi yao.

"Tunawaomba raia wa Burundi wanaoishi hapa nchini Tanzania, kurudi nyumbani ili tuijenge nchi yetu," alisema.

Aidha, ameishukuru Tanzania kwa kuwa jirani mwema na kuwapa hifadhi raia wa Burundi waliokimbia nchi yao.

Rais Magufuli amesisitiza ujumbe wa rais Nkurunziza na kuwataka wakimbizi hao kuchukua hatua za kurudi nyumbani kwa hiari.

"Rudini nyumbani kwa hiari, sisi hatutawafukuza," alisema rais Magufuli.

Mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kutoweka kwa mujibu wa Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za Binadamu kama Human Rights Watch.

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa ni mratibu wa mazugumzo ya kisiasa nchini humo, ambaye ameendelea kujaribu kuwaleta wapinzani wa kisiasa nchini humo kujaribu kuleta mwafaka wa kisiasa nchini humo.

Hata hivyo, kumekuwa na changamoto ya kuwakutanisha wanasiasa wa upinzani na viongozi wa serikali.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana