Pata taarifa kuu
KENYA-MAHAKAMA-SIASA

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya yaitaka IEBC kuendelea kuchapisha karatasi za urais

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imepata ahueni baada ya Mahakama ya rufaa kuamua kuwa inaweza kuendelea kuchapisha karatasi za kuwania urais kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.

Jengo la Mahakama jijini Nairobi nchini Kenya
Jengo la Mahakama jijini Nairobi nchini Kenya Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Majaji watano waliosikiliza rufaa ya kutaka kuruhisiwa kuendelea kuchapisha karatasi hizo, wamekosoa usitishwaji wa zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Al Ghurair ya Dubai, na hivyo haikuwa halali.

Jaji Eratus Githinji, akitoa uamuzi wa Mahakama hiyo kwa niaba ya wenzake, amesema kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu haukuzingatia muda mfupi unaosalia kwa nchi hiyo kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Huu ni uishindi mkubwa kwa Tume ya Uchaguzi ambayo sasa itaendelea na uchapishaji wa karatasi hizo kupitia kampuni hiyo ambayo muungano wa upinzani umesema kuwa haiaminiki.

Haijafahamika ikiwa upinzani utakwenda katika Mahakama ya juu kukata rufaa.

Mbali na hilo, mapema hivi leo  rais Uhuru Kenyatta amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki, anayezuru nchini Kenya na kudai kuwa upinzani unataka kuchelewesha Uchaguzi huo.

Faki amesema Umoja wa Afrika unataka Uchaguzi huo uwe huru na haki, siku ya Jumanne alikutana na mgombea wa upizani Raila Odinga.

Wakati uo huo, mgombea wa muungani wa upinzani Nasa Raila Odinga ametaja majina ya watu 42 ambao amesema wanatumiwa na serikali ya rais Uhuru Kenyatta kupanga kuiba kura.

Odinga amedai kuwa watu ni maafisa wa jeshi, usalama wa taifa na Polisi. Serikali imekuwa ikikanusha madai haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.