Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Rais Kiir atangaza hali ya hatari katika majimbo manne

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza hali ya hatari katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. REUTERS/Jok Solomon
Matangazo ya kibiashara

Kiir ametangaza hali hiyo katika majimbo manne ya Aweil Mashariki, Wau, Gogrial na Jonglei ambayo yameendelea kukabiliwa na utovu wa usalama.

Makabila yanayoishi katika majimbo hayo yamekuwa yakipigana na kusababisha mauaji na kuwaacha wenyeji wa majimbo hayo kukimbilia maeneo salama.

Wakati uo huo  msemaji wa serikali na Waziri wa Mambo ya ndani Michael Chiangjiek amesema hatua hii imechukuliwa baada ya thathmini ya kina lakini pia baada ya Baraza la Mawaziri kukutana na kuangalia hali ya kisiasa nchini humo.

Ripoti zinasema kuwa kwa wiki kadha zilizopita, watu 30 wamepoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa na ng'ombe zaidi ya 7,000 kuibiwa.

Sudan Kusini iliyoanza kujitawala mwaka 2011, imeendelea kukabiliana na utovu wa usalama nchini humo kuanzia mwaka 2013 baada ya waasi wanaoongozwa na Makamu wa rais wa zamani Riek Machar kuanza kukabiliana na vikosi vya serikali.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha nchini Sudan Kusini na wengine kuyakimbia makwao ikiwemo nchi jirani za Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Siku ya Jumapili kutakuwa na mkutano wa watalaam wa nchi za pembe ya Afrika IGAD, kuthathmini hali ya usalama nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.