Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Wanaochochea siasa kupitia Whatsapp nchini Kenya waonywa

Tume ya uwiano na utengamano wa kitaifa nchini Kenya inasema inachunguza makundi 21 ya Whatsapp yanayosambaza ujumbe wa chuki na uchochezi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.

Francis Ole Kaparo Mwenyekiti wa Tume ya uwiano na utengamano wa kitaifa
Francis Ole Kaparo Mwenyekiti wa Tume ya uwiano na utengamano wa kitaifa www.kbc.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Francis Ole Kaparo amesema, tayari wameanza mchakato wa kuwahoji wamiliki wa makundi hayo ya Whatsapp kutoka kaunti 21.

Kaparo amesema Tume yake itawafungulia mashtaka wale wote wanaochochea au kutuma ujumbe wa chuki kwa lengo la kuzua machafuko kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika tarehe nane.

Wakati uo huo, Tume ya Mawasiliano nchini humo imevitaka vyombo vya Habari nchini humo kutotangaza matokeo ya urais kabla ya Tume ya Uchaguzi kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Francis Wangusi amesema Tume hiyo inafahamu kuwa kuna vyombo vya Habari ambavyo vitakuwa vinajumuisha matokeo ya urais, na kuvitaka kutangaza matokeo yake baada ya IEBC kufanya hivyo.

Aidha, amesema kuwa Tume hiyo haina nia ya kufunga mitandao ya kijamii kama facebook,Twitter, Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.