Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Rais Kiir awafuta kazi Majaji 14 waliogoma kudai nyongeza ya mshahara

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewafuta kazi Majaji 14 waliokuwa wanagoma kwa muda wa miezi miwili sasa.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiir ametangaza hatua hiyo kupitia redio ya taifa, na kuwaambia raia wa Sudan Kusini kuwa Majaji hao wamefutwa kazi.

Inaaminiwa kuwa hatua hii imechukuliwa baada ya mgomo huo kukwamisha shughuli za Mahakama hiyo hasa jijini Juba.

Majaji hao wamekuwa wakigoma kushinikiza nyongeza ya mshahara lakini pia, kutaka kufutwa kazi kwa Jaji Mkuu Chan Reec Madut.

Madut amekuwa akishtumiwa na Majaji hao kwa kushindwa kuwatetea kuongezwa mshahara.

Mgomo huo ulimfanya rais Kiir kuunda Kamati ya kuchunguza kiini cha mgomo huo na mwezi uliopita, iliwasilisha ripoti yake kwa rais Kiir.

Hata kabla ya kufutwa kazi, Majaji hao waliamua kutorudi kazini hadi pale matakwa yao yangetekelezwa.

Majaji walioathiriwa na hatua hii ya rais Kiir ni pamoja na wale wa Mahakama ya rufaa, Khalid Mohamed Abdallah, Malek Mathiang Malek, Geri Raymondo Lege, George Anger Riing na Charles Abyei Jok.

Wale wa Mahakama kuu ni pamoja na, Nyok Monyrok Akwai, Awol Moyak Deng, Thor Andrew Makur, Geri Leon Wani, David Eriko Kati, George Phillip Laku na  Maker Tong Kiir.

Wengine ni pamoja ni pamoja na Bullen Isaiah Kulan na Paulino Duk Wayo.

Serikali ya Juba imekuwa ikikabiliana na mgawanyiko katika sekta ya umma tangu mwaka 2013 vita vilivyozuka kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wanaoongozwa na Riek Machar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.