Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini Rwanda zaanza

Kampeni za Uchaguzi Mkuu chini Rwanda zimeanza siku ya Ijumaa.

Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za rais wa Rwanda Paul Kagame
Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za rais wa Rwanda Paul Kagame twitter.com/newtimesrwanda
Matangazo ya kibiashara

Rais wa sasa Paul Kagame wa chama cha RFP, Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea binafsi Philippe Mpayimana wote kwa pamoja wamechagua kuanza kampeni zao nje ya jiji la Kigali.

Wagombea hawa wanatarajiwa kutumia siku 19 kuzunguka nchi nzima wakifanya mikutano ya hadhara na kuomba kuchaguliwa na wananchi wa Rwanda katika uchaguzi ambao hata hivyo rais Kagame anapewa nafasi ya kushinda kirahisi.

Rwanda bado inaendelea kupona majeraha ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, yaliyosababisha zaidi ya vifo vya Wanyarwanda 800,000.

Mgombea urais binafsi Philippe Mpayimana akiwa katika kampeni ya kukutana na wananchi katika wilaya ya Bugesera
Mgombea urais binafsi Philippe Mpayimana akiwa katika kampeni ya kukutana na wananchi katika wilaya ya Bugesera twitter.com/NewTimesRwanda

Tayari chama cha RPF cha rais Kagame, kimezindua manifesto yake kwa wananchi wa Rwanda na kuwaahidi kuendelea kuimarisha usalama wao, kujenga miundombinu muhimu lakini pia kuhimiza Umoja wa Taifa hilo.

Kampeni zinatarajiwa kumalizika tarehe 3 siku moja kabla ya wapiga kura wapatao Milioni 6.5 kupiga kura kuamua ni nani kati ya wagombea hao watatu, ataongoza nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.