Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Polisi nchini Kenya waanza operesheni ya kupambana na wezi wa mifugo

media Polisi wa kupambana na wezi wa mifugo nchini Kenya www.eyeradio.org

Serikali ya Kenya imetuma makumi ya polisi katika kaunti ya Lamu, baada ya maafisa usalama sita kupigwa risasi na kuuawa na wezi wa mifugo.

Afisa wa usalama ambaye hakutaka kufahamika, amesema mashambulizi ya angaa pia yatatumiwa kupambana na wezi hao wa mifugo.

Hii sio mara ya kwanza kwa wezi wa mifugo kukabiliana na maafisa wa Polisi na hata kuwauwa.

Mapema mwaka huu makabiliano makali yalizuka kati ya maafisa wa usalama na maelfu ya wezi hao wa mifugo wanaoaminiwa kutoka katika jamii ya Pokot.

Mwezi Aprili Tristan Voorspuy mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira raia wa Uingereza, alipigwa risasi na wezi hao wa mifugo na kupoteza maisha.

Mivutano ya kisiasa, eneo la kuchunga mifugo na mizozo ya umiliki wa ardhi ni sababu zinazoelezwa kusababisha mvutano huu.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana