Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Museveni ataka kuidhinisha miswada ya kuomba mikopo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemwandikia barua Spika wa bunge Rebecca Kadaga kumwagiza kuhakikisha kuwa mikopo yote ya serikali imfikie kabla ya kujadiliwa bungeni.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni DR
Matangazo ya kibiashara

Museveni ameelekeza kuwa mikopo 11 ya serikali iliyopelekwa bungeni ikataliwe kwa sababu haisadii kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Aidha, ameruhusu maombi 16 ya mikopo kupitishwa kwa sababu inalenga kuimarisha miundo mbinu kama barabara lakini pia kuinua sekta ya afya na elimu nchini humo.

Uganda ni mojawapo ya taifa la Afrika ambalo limekuwa likikopa sana na kufikia mwisho wa mwaka uliopita, nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilikuwa na deni la Dola Bilioni 8.7.

Waziri wa fedha Matia Kasaijja amekuwa akisema kuwa deni hilo ni sawa na asilimia 27 na hivyo kuipa nafasi ya kuendelea kukopa kwa maendeleo mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.