Pata taarifa kuu
KENYA

Mwanasiasa mkongwe nchini Kenya Nicholas Biwott afariki dunia

Wakenya wanaomboleza kifo cha Nicholas Kipyator Biwott, mwanasiasa mkongwe aliyekuwa Waziri wakati wa serikali ya rais Mustaafu Daniel Torotich Arap Moi.

Mwanasiasa wa siku nyingi Marehebu Nicholas Biwott
Mwanasiasa wa siku nyingi Marehebu Nicholas Biwott Yutube
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo alifariki dunia akiwa nyumbani kwake katika mtaa wa kifahari wa Kileleshwa jijini Nairobi.

Rais wa zamani Daniel Arap Moi aliyemteua Biwott katika nyadhifa mbalimbali, wakati akiwa rais kwa muda wa miaka 24, amesema amempoteza rafiki wa kweli aliyemtegemea sana.

Moi amesema Biwott aliyefahamika kwa jina maarufu la Total Man, alikuwa ni mtumishi wa serikali yake aliyejitolea sana kuwahudumia wakenya.

Amefariki dunia akiwa na miaka 77, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Wachambuzi wa siasa za Kenya na wale waliomfahamu wanasema kuwa, Biwot alikuwa ni mwanasiasa ambaye angeweza kukueleza  kwa undani historia ya uongozi wa Moi.

Alikuwa Mbunge kwa muda wa miaka 28 chini ya chama cha KANU, lakini baadaye akaunda chama chake cha National Vision Party of Kenya, ambacho kuelekea Uchaguzi wa mwezi ujao, kilitangaza kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.