Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Wagombea watatu kuwania urais nchini Rwanda mwezi Agosti

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda, imewaidhinisha wagombea wawili wa upinzani kupambana na rais Paul Kagame wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda Kalisa Mbanda
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda Kalisa Mbanda www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Profesa Kalisa Mbanda amesema wanasiasa hao wawili wa upinzani waliokidhi vigezo vya kuwania urais ni pamoja na Frank Habineza, kutoka chama cha Democratic Green Party na mgombea binafsi Philippe Mpayimana.

Gilbert Mwenedata, Fred Barafinda Skikubo na mwanamke wa pekee Diane Rwigara hawakufanikwia kuidhinishwa baada ya kukosa kupata saini za wapiga kura 600 kama inavyotakiwa kikatiba.

Tume hiyo mwezi uliopita, iliwapa siku tano wagombea hao kuhakikisha kuwa wanatimiza vigezo hivyo la sivyo wafungiwe kushiriki katika Uchaguzi huo.

Kigezo ambacho hawakutimiza ni kutopata sahihi za wapiga kura 600 kutoka kwa wilaya 12 kati ya 30 nchini humo.

Wagombea binafsi wamekuwa wakilalamikia kusumbuliwa na maafisa wa usalama katika harakati zao za kujitambulisha kwa raia wa nchi hiyo na kueleza mipango yao.

Kampeni zinatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.