Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Rais Kenyatta na Odinga wajiondoa kwenye mdahalo wa wagombea

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili na mpinzani wake wa karibu Raila Odinga kutoka muungano wa upinzani NASA, wametangaza kujiondoa kwenye mdahalo wa wagombea urais Jumatatu ijayo jijini Nairobi kuelekea Uchaguzi Mnkuu tarehe 8 mwezi ujao.

Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wagombea wakuu katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2017 nchini Kenya.
Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wagombea wakuu katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2017 nchini Kenya. DR.
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa chama rais Kenyatta cha Jubulee, Raphael Tuju amesema, waandalizi hao hawafanya mazungumzo yoyote na uongozi wa chama hicho kuhusu mdahalo huo.

Naye Salim Lon, mshauri wa Odinga amesema mgombea huy o yuko tayari kupambana na rais Kenyatta na wagombea wengine sita katika mdahalo huo lakini, hilo haliwezi kufanyika kwa mfumo ulioandaliwa.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya umepangwa kufanyika Agosti 8, na tayari Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu kutokea kwa vurugu kama zile zilizotokea miaka zaidi ya saba iliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.