Pata taarifa kuu
KENYA-EU-UCHAGUZI

EU yawatuma waangalizi wake Kenya

Nchini Kenya, ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa utulivu na kuheshimu demokrasia nchini humo zikisalia siku chahe kbala ya wa Uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 8. Ujumbe ulizinduliwa rasmi Jumatatu Julai 3 mjini Nairobi na utaundwa na idadi kubwa ya waangalizi kwa uchaguzi huo.

Agosti 8, wapiga kura wa Kenya watapiga kura hasa kumchagua rais wao na wabunge wapya.
Agosti 8, wapiga kura wa Kenya watapiga kura hasa kumchagua rais wao na wabunge wapya. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi thelathini waliwasili wiki iliyopita nchini Kenya, zaidi 32 wanatarajiwa siku chache kabla ya uchaguzi, lakini pia wataalam na wjumbe wengine wa Bunge la Ulaya. Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya kwa uchaguzi huo mkuu nchini Kenya utaundwa na watu 100 kwa jumla.

Uchaguzi huu ni muhimu kwa utulivu wa kanda nzima, alisema Marietje Schaake, mkuu wa ujumbe wa waangalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya. Ametolea wito vyama mbalimbali kuheshimu mchakato wa kidemokrasia. "Sio siri kuna wasiwasi kuhusu uwezekano wa mlipuko wa vurugu. Lakini hili halizuiliki. Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha wananchi wake haki ya kupiga kura kwa usalama na kwa mujibu wa chaguo lake, " Marietje Schaake amesema.

Miaka kumi iliopita, vurugu zilizuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, na kusababisha vifo vya watu 1000 na zaidi ya 600,000 kukimbia makazi yao. Leo, moja ya changamoto muhimu ni imani katika tume ya uchaguzi, iliokabiliwa siku za hivi karibuni na utata mkubwa.

"Watu wengi, ni lazima tuliseme, wametufahamisha kupitia maoni mbalimbali na ishara inayoonyesha ukosefu wa kujiamini, ameeongeza Marietje Schaake. Na tuangalia jinsi gani wasiwasi huu uko sahihi au la. "

Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya tarai amekutana na rais Uhuru Kenyatta, ambaye alimhakikishia kuchukua hatua zinazohitajika kwa kuhakikisha uchaguzi huru na wa wazi unafanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.