Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wanasiasa nchini Kenya wapigwa marufuku kutumia lugha za mama

Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya, imepiga marufuku vyama vya siasa nchini Kenya kutuma ujumbe mfupi kutumia lugha za mama au za kiasili.

Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya
Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya ca
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa kupambana na lugha za uchochezi kipindi hiki cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 8 mwezi Agosti.

Utaratibu huo uliotolewa na Tume hiyo ya Mawasiliano pamoja na Tume ya uwiano na utengamano, inavitaka vyama vya siasa nchini humo kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza pekee katika mawasiliano yake.

Aidha, lengo la utaratibu huu mpya ni kuwazuia wanasiasa kuepuka kutumia lugha ya uchochezi kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Whats App, Twitter na YouTube.

Kampuni za simu nchini humo sasa zitahitaji kupitia ujumbe uliotumwa na kuuwasilisha kwa mamlaka hayo ili kupitiwa kubaini ikiwa kuna matamshi ya uchochezi.

Mwaka 2007, wanasiasa walitumia lugha za mama kuchochea machafuko yaliyosababisha maafa ya watu na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.