Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Ahadi za rais Kenyatta kwa Wakenya ikiwa atachaguliwa tena

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili, ameanisha ilani ya chama chake cha Jubilee kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 8 mwezi Agosti.

Rais Uhuru Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili
Rais Uhuru Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili myuhurukenyatta/photos
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta ameahidi kuwa serikali yake itaunda nafasi mpya za kazi Milioni 6.5 kwa muda wa miaka mitano atakayokuwa madarakani.

Ameeleza kuwa hili litafanyika kwa kuhakikisha kuwa anajenga kiwanda kimoja katika Kaunti zote 47 nchini humo.

Elimu katika Shule za serikali za Sekondari itakuwa bure. Hakuna mwanafunzi yeyote atakayelipa ada ili kupata elimu.

Aidha, Kenyatta anaahidi kuimarisha sekta ya afya nchini humo kwa kupanua hospitali, kununua vifaa na kuinua kiwango cha tiba katika hospitali za serikali nchini humo.

Wanawake waja wazito nchini humo wataendelea kujifungua bure na kupata huduma muhimu bila malipo yoyote nchini humo kwa mujibu wa Ilani ya Jubilee.

Naibu rais William Ruto (Kushoto) akiwa na rais Uhuru Kenyatta (Kulia) wakati wa uzinduzi wa Ilani ya chama chao cha Jubilee Juni 26 2017 jijini Nairobi
Naibu rais William Ruto (Kushoto) akiwa na rais Uhuru Kenyatta (Kulia) wakati wa uzinduzi wa Ilani ya chama chao cha Jubilee Juni 26 2017 jijini Nairobi myuhurukenyatta/photos

Aidha, kiongozi huyo wa Jubilee ameahidi ikiwa atashinda atajenga makaazi ya bei nafuu 500,000 kote nchini lakini pia mabwawa ya maji 57 kwa lengo la kuimarisha sekta ya Kilimo nchini humo.

Pamoja hayo, Kenyatta amesema ikiwa atachaguliwa tena Wakenya wote wataunganishwa na nguvu za umeme kwa muda wa miaka mitatu ya uongozi wake.

Ahadi nyingine iliyotolewa na kiongozi huyu ni kujenga viwwanja  vipya vya kisasa vya michezo katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Mbali na ahadi hizi, rais Kenyatta amesema serikali yake inaimarisha usalama, kujenga reli ya kisasa lakini pia kuinua uchumi wa taifa hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.