Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania: Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yaonywa

Serikali ya Tanzania, inatishia kuyafungia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yatakayokwenda kinyume na uamuzi wa rais John Magufuli kwa kuwazuia wasichana wajazito kuendelea na masomo ya shule za msingi na Sekondari.

Rais wa Tanzania John Magufuli
Rais wa Tanzania John Magufuli AFP Photo/Daniel Hayduk
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya ndani nchini humo Mwigulu Nchemba amesema serikali ya rais Magufuli hatarudi nyuma katika uamuzi huo uliochukuliwa na kiongozi wa nchi hiyo wiki iliyopita.

Amesisitiza kuwa mjadala kuhusu wasichana hao, umefungwa rasmi na rais Magufuli.

Kauli ya rais Magufuli imezua mjadala mkubwa nchini humo hasa miongoni mwa wanaharakati waliolaani uamuzi huo.

Mashirika hayo ya kiserikali pamoja na wanaharakati wa wanawake nchini humo na barani Affrika, wameanzisha harakati za kukusanya sahihi za kumtaka rais Magufuli kuomba radhi na kubadilisha uamuzi wake.

Serikali ya Magufuli imeendelea kutoa elimu ya bure kwa wanafunzi nchini humo wanaosoma katika shule za serikali, shule za msingi na sekondari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.