Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

EU kuipa Uganda Euro Milioni 85 kushughulikia wakimbizi

media Antonio Guterres (kushoto) na mkurugenzi wa shirika la mpango wa Chakula Duniani (WFP), wakigawa chakula kwa wakimbizi katika mji wa Imvepi June 22. RFI / Charlotte Cosset

Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa Euro Milioni 85 kwa nchi ya Uganda kusaidia kuwashughulikia zaidi ya wakimbizi Milioni moja nchini humo.

Ahadi hii imetolewa katika kongamano la siku mbili kuhusu wakimbizi linalomalizika leo jijini Kampala.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amewatembelea wakimbizi wa Sudan Kusini Kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka machafuko kumalizika katika taifa hilo ili kuepusha raia wa nchi hiyo kuyakimbia makwao.

Kupitia kongamano hili, Uganda inatarajiwa kupata Dila Bilioni 2 kusaidia kuwahifadhi wakimbizi hao.

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Uganda kwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi Milioni 1.2 kutoka Sudan Kusini , Burundi , Rwanda , Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini inaelemewa na gharama za kuwasaidia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana