Pata taarifa kuu
UGANDA-WAKIMBIZI

Kongamano la kimataifa kuhusu wakimbizi lafanyika nchini Uganda

Kongamano la siku mbili la Kimataifa kutafuta njia za kuwasaidia wakizmbi nchini Uganda linaanza leo jijini Kampala. Uganda inawapa hifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani kama vile Sudan kusini, Rwanda, Burundi na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Uganda imeendelea kuwapa hifadhi wakimbizi kutoka mataifa jirani.
Uganda imeendelea kuwapa hifadhi wakimbizi kutoka mataifa jirani. AFP PHOTO / UNMISS/BEATRICE MATEGWA
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ndio mgeni rasmi katika kongamano hilo ambalo mwenyeji wake ni rais Yoweri Museveni.

Wajumbe na watalaam mbalimbali pia wapo jijini Kampala kujadili suala hili.

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Uganda kwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi Milioni 1.2 kutoka Sudan Kusini , Burundi , Rwanda , Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini inaelemewa na gharama za kuwasaidia.

Soma zaidi hapa.Bonyeza hapa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.