Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UN

UN yasema Sudan Kusini sasa haikabiliani na njaa kali

Umoja wa Mataifa unasema taifa la Sudan Kusini sasa halikabiliani tena na baa kubwa la njaa.

Raia wa Sudan Kusini wakiwa wamebeba msaada wa chakula
Raia wa Sudan Kusini wakiwa wamebeba msaada wa chakula Albert Gonzalez Farran / Albert Gonzalez Farran - AFP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za UN zimesema hatua hii imekuja kutokana na ongezeko la misaada ya kibinadamu nchini humo katika siku za hivi karibuni.

Hata hivyo, UN inasema hali bado ni mbaya kwa sababu raia wengi wa nchi hiyo wanahitaji chakula na misaada mingine ya kibinadamu kama dawa.

Mapigano ya mara kwa mara nchini humo, kutokuwa na mavuno mazuri mashambani, kupanda kwa bei ya vyakula, vimeelezwa kuwa sababu ya hali hii ya ukame.

Mzozo nchini Sudan Kusini umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na Mamilioni kuyakimbia makwao na kusalia wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.