Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHUMI=MAFUTA

Serikali ya Burundi kudhibiti tatizo la uhaba wa mafuta

Serikali ya Burundi, imeanza kushughulikia tatizo la uhaba wa mafuta ambao ulijitokea nchini humo tangu miezi mitatu iliyopita. Tangu siku ya Alhamisi jioni misururu ya magari mbele ya vituo vya mafuta haipo tena.

Mafuta yameanza kupatikana katika vituo mbalimbali vya mkuu mkuu wa Burundi, Bujumbura.
Mafuta yameanza kupatikana katika vituo mbalimbali vya mkuu mkuu wa Burundi, Bujumbura. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, hivi karibuni Umoja wa Ulaya ulitenga Euro milioni 23 ulizokua ukidaiwa na askari wa Burundi wanaoshiriki katika tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Somalia. Kutokana na malipo hayo, Burundi imekusanya dola milioni 12 ili kuagiza nje mafuta kwa minajili ya kukabiliana na uhaba wa bidhaa hiyo nchini humo. Lakini wadadisi wanasema kiwango kilichotumwa ni kidogo mno na hakiwezi kuzidisha mwezi mmoja.

Malimbikizo haya ya mishahara ilizuiliwa kwa muda wa mwaka mmoja, baada ya Umoja wa Ulaya kuchukua uamuzi wa kusitisha misaada yake kwa Burundi kutokana na utawala wa Pierre Nkurunziza kuendelea kuvunja haki za binadamu na kukataa kushiriki mazungumzo baina ya Warundi katika hali ya kutafutia ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa uliojitokea kufuatia uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhala wa tatu, jambo ambalo ni kinyume cha mkataba wa amani wa Arusha uliopelekea kusimama kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu zaidi ya mwongo mmoja, kwa mujibu wa mashirika mbalimbali ya kiraia.

Kutokana na uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya, uchumi wa Burundi umefiki pabaya, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa mafuta kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni nchini.

Itakumbukwa kwamba kulikua na mvutano kati ya serikali ya Burundi na Umoja wa Ulaya, ambapo Umoja huo ulitaka mishahara ya askari wa Burundi waliopo Somalia iwekwe katika akaunti zao binafsi na kwenye benki za kibinafsi, huku serikali ya Burundi ikitaka mishahara hiyo ilipwe kupitia akaunti za serikali.

Baada ya hapo, pande zote mbili zilikubaliana kuwa mishahara ya askari wa Burundi waliopo nchini Somalia iwekwe kwenye akaunti zao zilizofunguliwa kwenye benki ya kibiashara ya Burundi, BANCOBU, huku serikali ikinufaika kwa zaidi ya 20% kama ilivyokua hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.