Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAREKANI

Marekani kutoa Dola Milioni 526 kwa Tanzania kupambana na maambukizi ya UKIMWI

Marekani itatoa msaada wa Dola Milioni 526 kwa nchi ya Tanzania kusaidia kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

Mfano wa upimaji wa maambukizi na virusi vya HIV
Mfano wa upimaji wa maambukizi na virusi vya HIV REUTERS/Dinuka Liyanawatte
Matangazo ya kibiashara

Ubalozi wa Marekani nchini humo umesema fedha hizo zitaingia nchini Tanzania mwaka ujao, kwa lengo la kununua dawa za ARV'S kuwasaidia watu walioambukizwa.

Takwimu zinaonesha kuwa watu Milioni 1.4 katika taifa hilo la watu Milioni 50 wameambukizwa na ugonjwa huu ambao bado hauna dawa na hatua ya Marekani ni faraja kubwa kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

Tanzania kupata fedha hizi, kunamaanisha kuwa watu watakaokuwa na uwezo wa kupata dawa za ARV'S watafikia Milioni 1.2.

Msaada huu ni ongezeko kwa asilimia 12 iliyotolewa mwaka uliopita, na pamoja na kununua dawa zinazotolewa bure kwa wagonjwa, itasaidia pia watu wengine Milioni 8.6 kupimwa hali yao ya HIV.

Inaripotiwa kuwa watu karibu 360,000 huambukizwa HIV kila mwaka, na msaada huu unakuja kwa wakati mwafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.