Al Shabab yawauawa watu wawili Kaskazini Mashariki mwa Kenya
Watu wawili akiwemo afisa wa serikali wameuawa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab katika kaunti ya Mandera Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Maafisa nchini Kenya wanasema watu hao walitekwa kabla ya kuuawa na wanamgambo hao waliokimbilia nchini Somalia.
Polisi wamesema tayari maafisa wa usalama wametumwa katika eneo hilo kudhibiti usalama wakati huu msako mkali ukiendelea kuwatafuta magaidi hao.
Hii ndio mara ya kwanza ndani ya muda mrefu kwa ripoti za uvamizi wa Al Shabab kuripotiwa katika eneo hilo ambalo limekuwa chini ya ulinzi mkali.
Kundi la Al Shabab limeendelea kuwa hatari kwa serikali ya Kenya na usalama wa Afrika Mashariki.
Kenya ni miongoni mwa mataifa ambayo yametuma vikosi vyake nchini Somalia chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika AMISOM tangu mwaka 2011 kupambana na Al Shabab.