Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI

Miili ya wanafunzi na waalimu waliopoteza maisha Tanzania kuagwa Jumatatu hii

Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Visent jijini Arusha.

Ni katika mji wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania ambako ibada na dua za kuaga miili ya wanafunzi n waalimu pamoja na dereva wa basi itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Ni katika mji wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania ambako ibada na dua za kuaga miili ya wanafunzi n waalimu pamoja na dereva wa basi itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. © Photo: Wikimedia/Phase9
Matangazo ya kibiashara

watu hao walipotezamaisha katika ajali iliyotokea Mei 6, 2017 katika eneo la Rhotia mkoani Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi Jumatatu hii Mei 8 saa za Afrika Mashariki.

Wanafunzi na walimu hao walipoteza maisha katika ajali wakati walipokua wakisafiri kuelekea shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Imebainika kuwa wanafunzi waliopoteza maisha walikuwa ni wa darasa la saba kutoka shule ya kibinafsi ya LackVicent yenye makao yake mjini Arusha.

Baada ya ajali hiyo mbaya kutokea, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alisema amesikitishwa sana na mkasa huo na kutuma salamu za pole kwa jamaa ndugu na marafiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.