Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Kenya: Odinga ateuliwa na muungano wa NASA kugombea urais Agosti 8

Muungano wa upinzani nchini Kenya wa NASA umemtangaza aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga kuwa mgombea wake wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu.

Raila Odinga ambaye amechaguliwa na muungano wa NASA kupeperusha bendera ya muungano huo kwenye uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu.
Raila Odinga ambaye amechaguliwa na muungano wa NASA kupeperusha bendera ya muungano huo kwenye uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Muungano huo pia umemtangaza aliyewahi kuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka kuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Vinara hawa watano wa upinzani wanatumaini kuwa muungano wao utatosha kukishinda chama tawala wa Jubilee wakati wa uchaguzi wa mwezi wa 8 mwaka huu.

Maelfu ya wafuasi wa muungano huo walijitokeza kwenye viwanja vya bustani ya Uhuru jijini Nairobi kushuhudia muungano wao ukimtangaza mtu atakae peperusha bendera ya urais kupambana na Uhuru Kenyatta.

Ikiwa kama marejeo ya kile kilichofanyika mwaka 2013, Kalonzo Musyoka alitangazwa kuwa mgombea mwenza ambaye ikiwa watashinda atakuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.

Nafasi nyingine za uongozi ndani ya muungano huo ziligawanywa kwa wanasiasa wengine ambao ni Musalia Mudavadi, Moses Wetangula na Issack Ruto.

Akizungumza kabla ya kumtangaza mgombea wao, kinara wa chama cha Amani Musalia Mudavadi alisema yeye binafsi pamoja na wenzake wamejitoa kwaajili ya kuiunganisha nchi na kuondoa madhila yanayowakabili wananchi.

"Wajumbe wote wa NASA wako sawa na hakuna atakayekuwa anajifanya kuwa mbele kuliko wengine." alisema Mudavadi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.