Pata taarifa kuu
TANZANIA-MUUNGANO

Magufuli: Mafanikio ya muungano ni juhudi za viongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ameonya yeyote yule atakayejaribu kuvunja muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar, akisema kuwa muungano huo umepatikana kwa juhudi za viongozi na waasisi wa muungano huo.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Tahadhari hiyo ameitoa siku ya Jumatano Apili 26, mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika mjini Dodoma.
Rais John Pombe Magufuli amesema mafanikio yaliyopatikana kutokana na muungano yamefaanikishwa kwa juhudi za viongozi wa taifa na waasisi wa muungano.

Rais Magufuli amesema muungano huo umefanikiwa kwani mpaka sasa nchi za Unguja na Tanganyika zimetawaliwa na amani

Aidha Rais Magufuli amekiri kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto mbalimbali zinazoukabili Muungano huo.

Wakati huo huo rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 2,219 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya muungano.

Wafungwa hao ni wale wenye magonjwa kama Ukimwi, Saratani na Kifua Kikuu na wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani, Projest Rwegasira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.