Pata taarifa kuu
TANZANIA-UNDP-USHIRIKIANO

Magufuli amfukuza mkuu wa UNDP nchini Tanzania

Serikali ya Tanzania imechukua uamuzi wa kumfukua Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo (UNDP), anayetuhumiwa kuwa kikzwa katika shughuli za shirika hilo nchini Tanzania.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amtimua Mkurugenzi Mkuu mwakilishi wa UNDP Tanzania.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amtimua Mkurugenzi Mkuu mwakilishi wa UNDP Tanzania. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania amesema Awa Dabo, raia kutoka Gambia, amekuwa na mahusiano ya mvutano na wenzake kutoka shirika hilo la Umoja wa Mataifa na kwa hiyoametakiwa kuondoka nchini Tanzania.

Bi Dabo, ambaye tayari ameondoka nchini humo, alikua amepewa muda wa saa 24 awe ameshaondoka nchini Tanzania.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje inasema kuwa usimamizi mkali wa Bi Dabo ulizuiwa shughuli ya shirika hilo kutendeka vizuri.

"Uwepo wake ulikuwa kikwazo kwa juhudi za maendeleo ya nchi," taarifa ya wizara imesema.

Tanzania imeomba UNDP kuwakumbusha wafanyakazi wake kwamba kipaumbele chao cha kwanza ni kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo endelevu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.