Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

UN: tunatiwa wasiwasi na itikadi na wito wa chuki na vurugu Burundi

media Nchini Burundi, Imbonerakure wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali vya ukatili dhidi ya raia. RFI

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inalaani uchochezi wa chuki na vurugu katika mikutano inayoendeshwa katika mikoa kadhaa ya Burundi. Kwa mujibu wa OHCHR, Imbonerakure, vijana kutoka chama tawala cha CNDD-FDD, lakini pia viongozi wa chama tawala au viongozi tawala wamekua wakitoa kauli hizo.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imenyooshea kidolea cha lawama viongozi hao kufanya kampeni ya kuwafanyia vitisho wananchi wa Burundi. Mamia ya vijana wa chama cha CNDD-FDD, Imbonerakure, mara kwa mara wame kua wakimba nyimbo zinazotolea wito wa kuwapa ujauzito wanawake kutoka vyama vya upinzani na kuwaua wanaume wote kutoka vyama hivyo, bila hata hivyo kuchukuliwa hatua.

Gavana wa mkoa wa Makamba au rais baraza la Seneti, Reverien Ndikuriyo, mwenyewe pia alitoa kauli za kuchochea chuki.

Scott Campbell, mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, katika kanda ya Afrika ya kati, amesema "maneno haya ni ya kutisha na tuna wasiwasi kutokana na maneno haya, hasa katika eneo ambalo hujulikana sana kwa mauaji mengi yaliyotokea hivi karibuni". Ameomba jumuiya ya kimataifa kutathimini kauli hizo. "Ni vizuri kuonyesha msimamo wetu sasa. Bila kukomesha ukatili, nchi inaweza kukumbwa na machafuko mabaya zaidi, " amesema Scott Campbell.

Mapema mwezi Aprili, chama tawala cha CNDD-FDD, kililaani baadhi ya nyimbo hizo. Lakini Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inasema kuwa kampeni hizo zinaendelea bila wasiwasi wowoote. Gaston Sindimwo, Makamu wa rais, hajakanusha lakini amepuuzia mbali madai hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana