Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Rais Magufuli alaani mauaji ya Polisi 8 Pwani ya nchi hiyo

media Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli AFP Photo/Daniel Hayduk

Rais wa Tanzania John Magufuli amelaani kuuawa kwa Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha siku ya Alhamisi eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani nchini humo.

Ripoti zinasema Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wakati waliposhambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Magufuli amesema ameshtushwa na kusikitishwa sana na vifo vya askari hao waliokuwa wanalitumikia taifa hilo.

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu.

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi wa nchi hiyo ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana na maafisa wa Polisi ili kukomesha mauaji kama haya.

Hii sio mara ya kwanza, kwa maafisa wa Polisi kushambuliwa Pwani ya nchi hiyo na kuzua hali ya wasiwasi.

Mwaka 2015, watu waliokuwa na silaha walivamia kituo cha polisi jijini Dar es salaam na kuwauawa maafisa wanne wa polisi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana