Pata taarifa kuu
RWANDA

Rais Kagame alaani wanaopotosha historia ya mauaji ya kimbari nchini mwake

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema ni upuuzi kujaribu kutoa jina kwa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini mwake mwaka 1994 na kusababisha vifo vya watu 800,000.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ( Kulia) na mkewe pamoja na Moussa Faki Mahamat(Kushoto) wakitoa heshima katika eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbarai nchini humo siku ya Ijumaa Aprili 7 2017
Rais wa Rwanda Paul Kagame ( Kulia) na mkewe pamoja na Moussa Faki Mahamat(Kushoto) wakitoa heshima katika eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbarai nchini humo siku ya Ijumaa Aprili 7 2017 Rwanda Presidenct Twitter
Matangazo ya kibiashara

Akionekana mwenye hasira wakati wa akihutubia kwenye siku ya kuanza juma la maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 23 ya mauaji hayo, rais Kagame amesisitiza kuwa watu wanaojitosa katika mjadala wa jina la mauaji hayo ni wapuuzi.

Hata hivyo, rais Kagame amesema hakuna haja ya kuficha ukweli kuwa wengi ya watu waliouawa walikuwa ni wa jamii ya watutsi walioanza kulengwa hata kabla ya mauaji yenyewe ya mwaka 1994.

“Tusema ukweli kuwa Watusti ndio waliolengwa katika mauaji hayo hata kabla ya mwaka 1994, natumai kuwa hamjasahau, nasema haya ili kuwakumbusha watu historia na kuweka kumbukumbu vizuri kama wengi hatukumbuki,” alisema Kagame.

“Ni upuzi mkubwa sana kuwaona watu wakijaribu kujiuliza, ikiwa mauaji haya yalikuwa dhidi ya Watutsi au Wahutu wenye msimamo wa kati,” aliongeza.

“Waliopoteza maisha ni raia wa Rwanda na wanaojihusisha na mjadala huu kuna wengine walihusika,”.

Kagame ameeleza kuwa hakuna wakati mwingine nchi hiyo itashuhudia mauaji mabaya kama hayo, na wakati huo huo akitoa wito kwa Wanyarwanda kusonga mbele na kuendeleza gurudumu la maisha.

“Mauaji haya yalitokea, hakuna anayeweza kuwarudisha watu wetu waliopoteza maisha, inabidi tusonge mbele,”.

''Lazima tukubali kuwa hakuna kilichofanyika kuzuia mauaji haya,” alisisitiza.

Kiongozi huyo ameogeza kuwa nchi yake inapiga hatua za kimaendeleo na kuyataka mataifa yanayotaka kushirkiana na Rwanda kujitokeza ili kuimarisha ushirikiano huu.

Kumbukumbu ya mwaka huu imekuja baada ya rais Kagame hivi karibuni kukutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ambaye aliomba radhi kwa Kanisa kushindwa kuzuia mauaji hayo na baadhi ya Makasisi wake kuhusika.

Rais Kagame amesema amefurahi kwakuwa kanisa katoliki limekubali kuwa baadhi ya viongozi wake walihusika na limeomba radhi.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat pia alihudhuria kumbukumbu hii jijini Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.