Pata taarifa kuu
UGANDA

Museveni adai wanasiasa wa upinzani wanataka kuiangusha serikali yake

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amedai kuwa wanasiasa wa upinzani wanapanga kuiangusha serikali yake.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ©Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Museveni ameeleza kuwa anastaajabishwa sana na shinikizo za wanasiasa hao wanaomtaka kutekeleza kila kitu kwa wakati mmoja.

Kiongozi huyo ambaye amekuwa uongozini kwa miaka 30, amewataka wabunge wa chama tawala NRM, ni lazima wawe makini na wabunge wa upinzani.

“Wanataka tushike hapa na pale, bila kumaliza kazi yoyote. Sisi tunataka tufanye kazi hatua kwa hatua,” alisema Museveni.

Aidha, amesema kuwa kuongoza serikali sio jambo rahisi na kusisitiza kuwa kila mtu ana namna yake ya kuongoza.

Museveni amewaambia wafuasi wa chama chake kuwa, serikali yake imefanikiwa kuleta amani, kuimarisha sekta ya afya nchini humo.

Upinzani nchini Uganda ukiongozwa na Kizza Besigye amekuwa akimkosoa rais Museveni na kusema ni dikteta ambaye ameshindwa kuongoza nchi hiyo.

Kumekuwa na ripoti kuwa huenda rais Museveni na Besigye wakashiriki katika mazungumzo ya kisiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.