Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Jukwaa la kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania latamatika jijini Dar

media Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak akifanya mahojiano na mwandishi wa rfikiswahili (hayuko pichani). April 6, 2017, RFI

Mkutano wa kwanza wa aina yake wa jukwaa la kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania, umetamatika jijini Dar es Salaam Tanzania, huku Serikali ya Ufaransa ikieleza kuridhishwa na namna ambavyo nchi ya Tanzania imeanza kutekeleza kwa vitendo sera ya kuelekea nchi ya viwanda.

Mkutano huu wa siku nne uliwakutanisha wadau kutoka Ufaransa na wale wa Tanzania, ambapo walibadilishana mawazo na ujuzi kuhusu shughuli mbalimbali za uwekezaji hasa kwenye sekta za miundombinu kama barabara, reli, usafiri wa anga, utalii, teknolojia ya mawasiliano na nishati.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na idhaa ya rfikiswahili, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak, amesema amfurahishwa sana na namna ambavyo Serikali ya Tanzania pamoja na wadau kutoka sekta binafsi jinsi walivyoshiriki mkutano huu.

Balozi Berak amesema licha ya kuwa mkutano huu ni wa kwanza kuandaliwa na nchi yake, anaamini wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa Ufaransa wamenufaika kupitia jukwaa hili adimu na la kipekee kwa nchi ya Ufaransa.

“Kusema kweli imenishangaza kidogo, sikutarajia kabisa kama ushiriki wa wadau wa sekta binafsi na Serikali ya Tanzania wangeshiriki kwa wingi hivi hasa ukizingatia kuwa huu ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa aina hii.” alisema balozi Berak.

Ameongeza kuwa “napenda niwapongeze wadau kutoka Tanzania na hata wale wa Ufaransa walioshiriki mkutano huu”.

Alipoulizwa na mwandishi wa idhaa hii kuhusu namna ambavyo ameona makampuni ya Ufaransa yameuchukulia mkutano huu, balozi Berak amesema amepata maoni chanya kuhusu mijadala iliyokuwa ikiendelea wakati wa mkutano na kwamba ni imani yake kuwa huu hautakuwa mkutano wa mwisho wa aina hii kufanyika Tanzania.

Balozi Berak amesema mkutano huu ulikuwa na fursa nyingi ambazo ikiwa makampuni ya Ufaransa yatazitumia basi sio ajabu wakaubadilisha sana uchumi wa taifa la Tanzania kupitia uwekezaji.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak akihojiwa na idhaa ya rfikiswahili wakati wa mkutano wa jukwaa la kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania. April 6, 2017. RFI

Kuhusu changamoto ambazo wadau wa Ufaransa wamemueleza, Balozi Berak amesema ni kweli kuwa ili uwekezaji wowote uwe wa mafanikio ni lazima nchi husika ihakikishe kuwa mazingira yanakuwa ya kuvutia na kuwarahishia wale wanaotaka kuja kuwekeza Tanzania.

Amesema kuwa “Ni kweli Tanzania ina usalama wa uhakika na hali ya siasa iliyotulia, jambo ambalo ni muhimu sana kwa wawekezaji, lakini ifahamike kuwa ili mwekezaji avutiwe ni lazima vile vikwazo kama sera za kodi zenye utata, usajili wa kampuni na vibali vya kazi ni lazima viondolewe au vihusianishwe na wakati uliopo.

Amedai Tanzania ina maeneo mengi ya fursa ambayo Ufaransa itahakikisha inajaribu kuzitumia kama vile kwenye sekta ya nishati na madini pamoja na miundombinu, maeneo makuu ambayo amesema anaona yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sekta za uma, binafsi na Serikali.

Nao wadau kutoka sekta binafsi hasa kupitia mwenyekiti wake Reginald Mengi, amesema wafanyabiashara kutoka Tanzania wanajivunia kushiriki kwenye mkutano huu na wamejifunza mambo ambayo wataanza kuyafanyika kazi ili kuleta muunganiko mzuri kati yao na wale wa Ufaransa.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi kutoka nchini Tanzania, wanasema ikiwa Serikali za Afrika Mashariki hazipambana na vitendo vya rushwa, kuimarisha demokrasia na utawala bora na kudhibiti hali ya usalama na amani kwenye nchi zao, itakuwa vigumu sana kwa wawekezaji hawa kurejea.

Wengi wanaona kuwa Ufaransa imefanikiwa sana kwenye sekta ya utalii, viwanda na kwenye miundombinu maeneo ambayo nchi kama ya Tanzania inayoelekea kwenye kipato cha kati na nchi ya viwanda inahitaji usaidizi kutoka kwa wataalamu wa Ufaransa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana