Pata taarifa kuu
BURUNDI - SIASA

Chama cha CNDD-FDD cha laumiwa kuwatoza kodi raia wa Cibitoke bila khiari

Wananchi wakaazi wa Mkoa wa Cibitoke kaskazini Magharibi mwa Burundi, wanakilalamikia chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD kwa kuwatoza kodi kwa nguvu kwa ajili ya ujenzi wa Makao makuu ya chama hicho bila kujali ni mwanachama wake au la. hayo yanajiri wakati huu kukiripotiwa hali ya kiuchumi miongoni mwa wananchi ikiwa ni madhara ya vurugu za kisiasa zilizoikumba nchi hiyo sasa ni miaka miwili. 

Wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD
Wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD AFP / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda wengi walioongea kwa njia ya simu na RFI wanasema wamepatwa na hasira na wanachanganyikiwa kwani hawalewi kwanini wanatozwa michango kwa nguvu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama tawala na ilihali sio wanachama wa CNDD-FDD.

Kila mwanachi anatakiwa kulipa mchango kutokana na kazi yake, mathalan mwananchi wa kawaida analipia kiwango cha chini ya Euro moja, muendesha boda boda anatozwa Euro 4 wakati mfanyabiashara akitakiwa kulipa Euro 40 hadi 80. ikiwa ni kiwango kikubwa mno ukilinganisha na hali mbaya maisha nchini humo.

Mashahidi nchini humo wanasema, ukiuliza kwanini umekatwa kiwango cha fedha, unaambiwa ni amti kutoka katika chama tawala, na kama hutaki unaweza kuhiunga na wengine walioitoroka nchi.

Kwa sasa zaidi ya watu laki nne waliitoroka nchi kufuatia mzozo wa kisiasa ulioibuka humo sasa ni miaka 2.

kwa mujibu wa mtandao wa habari wa SOS-Burundi, katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD ngazi ya mkoa Alfred Nsekambabaye alieleza kwamba makao makuu ya chama tawala hivyo ni sehemu ya majengo ya taifa. Kiongozi mmoja wa chama ambae aliahidi kuliweka wazi swala hili hatimae hakupatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.