Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Tanzania: Wawekezaji wa Ufaransa wasiogope kuja mazingira yanaruhusu

media Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa. April 3, 2017. Tanzania/VPO

Serikali ya Tanzania imesema imeboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya uwekezaji na kwamba hakuna sababu ya wawekezaji kutoka mataifa ya Ulaya na hasa Ufaransa kwenda kuwekeza nchini humo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza na waina yake wa jukwaa la kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa, makamu wa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali iliyopo madarakani itahakikisha inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuvutia wafanyabiashara zaidi.

Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali tayari imeanza kutoa kipaumbele kwenye uwekezaji wa ardhi na kwamba kuna maeneo makubwa yametengwa kwaajili ya kilimo ambapo ameongeza kuwa hii ni fursa kwa Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania.

Samia ameongeza kuwa nchi ya Tanzania imeanza safari ya kuelekea kuwa nchi ya viwanda na kwamba kila mwaka Serikali imetenga bajeti kwaajili ya kuboresha miundombinu inayohusu nishati, maji, barabara, bandari na reli.

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu (mwenye hijabu) akiwa na balozi wa Ufaransa Tanzania, Malika Berak. April 3, 2017 Emmanuel Makundi/RFIKIswahili

“Kwa miaka sasa Serikali imekuwa ikifurahia uchumi uliojikita kwenye masoko ambapo nchi ilikuwa ikiratibu na kuwa mstari wa mbele katika kusimamia wakati sekta binafsi ikiwa chachu ya mabadiliko na injini ya ukuaji wa uchumi,” alisema makamu wa rais Samia Suluhu.

Makamu wa rais huyo ameongeza kuwa kwa kuona umuhimu wa Sekta binafsi kushirikishwa kwenye ukuzaji wa uchumi wa nchi, Serikali imeendelea kushirikiana na sekta hiyo kuhakikisha wanafanya kazi bega kwa bega na kuondoa ukiritimba uliokuwepo kwa wawekezaji wa ndani na wale wa nje.

Ameongeza baada ya kubaini uwepo wa changamoto mbalimbali za kiuwekezaji hasa kwa wageni, Serikali imekuwa ikitoa msaada mkubwa wa kuratibu masuala ya usajili wa kampuni kwa wawekezaji, uhamiaji, ajira, ardhi, kodi na leseni ya biashara kupitia vituo maalumu.

Makamu wa rais Samia Suluhu amesema kuwa amani na utulivu ulipo nchini Tanzania inatosha kuwashawishi wawekezaji wa kimataifa na hasa wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuja kuwekeza kwenye taifa hilo.

Kwa upande wake balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak, amesema mkutano huu ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania na kwamba nchi ya Ufaransa inafahamu fursa zilizoko Tanzania na ndio maana wakasisitiza mkutano huu kufanyika wakati huu.

Balozi Berak amesema wakati wa mkutano huu, wafanyabiashara wa Ufaransa na wale wa Tanzania watabalishana mawazo na ujuzi na kubainisha maeneo ambayo watashirikiana ili kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili.

“Makampuni zaidi ya 50, wakurugenzi wake na wafanyabiashara kutoka Ufaransa na Afrika wanashiriki kwenye mkutano huu muhimu ambao utaunganisha tamaduni za nchi hizi na kukuza mahusiano ya kibiashara,” alisema balozi Berak.

Balozi Berak ametaka kongamano hili litumiwe kikamilifu na washiriki na hasa wawakilishi kutoka Serikalini kwa kuwa sekta ambazo zitajadiliwa zinagusa maeneo muhimu ambayo Tanzania kwa muda mrefu imeonesha juhudi za kutaka kutatua kero za wananchi wake hasa kwenye nishati, barabara, reli na mawasiliano.

“Tunapenda kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kushirikiana nasi kuhakikisha mkutano huu unakuwa wa mafanikio, hii inaonesha ni kwa namna gani nchi ilivyotayari kushirikiana na Ufaransa kibiashara, kiuchumi na kitamaduni”. Alimaliza balozi Berak.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa sekta binafsi nchini Tanzania TPSF, Godfrey Simbeye, akizungumza kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wa RFI Kiswahili, amesema mkutano huu utakuwa chachu kwa wafanyabiashara nchini kutazama fursa zilizoko nchini Ufaransa na Ufaransa kutumia fursa zilizoko Tanzania.

Simbeye amesema ni jambo jema kuona sasa Ufaransa inabadili uelekeo wa sera zake za kigeni hasa kwenye uwekezaji na kufanya biashara na nchi kama Tanzania.

“Unajua Ufaransa ilikuwa imejikita na pengine ilijisahau sana na kutoa kipaumbele kikubwa kwa nchi ambazo zilikuwa ni makoloni yake na kusahau nchi nyingine kama Tanzania, nadhani sasa wameona fursa zilizoko Tanzania na ndio maana sasa wameamua kujaribu nchini Tanzania, kwa hivyo ni fursa ya aina yake kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana