Pata taarifa kuu
KENYA

Bajeti nchini Kenya yawasilishwa mapema kwa sababu ya Uchaguzi Mkuu

Bajeti ya kifedha ya mwaka 2017-2018, inawasilishwa leo nchini Kenya.

Waziri wa fedha wa Kenya Henry Rotich
Waziri wa fedha wa Kenya Henry Rotich Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa fedha Henry Rotich anakwenda bungeni na Bajeti ya Shilingi za Kenya Trilioni 2.6, ikiwa ndio bajeti kubwa zaidi kushuhudia nchini humo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa bajeti nchini Kenya kuwasilishwa kwa wabunge mwezi Machi.

Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini yamekuwa yakiwasilisha bajeti zao kwa pamoja mwezi Juni utaratibu ambao Kenya itarejesha mwaka 2018.

Hata hivyo, hali imekuwa tofauti nchini Kenya kwa sababu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Wabunge wengi nchini humo huenda wasiwe bungeni mwezi Aprili kuandaa bajeti hiyo kwa sababu za kisiasa, na ikiwa bajeti haingewasilishwa mapema, basi ingeathirika.

Wizara ya fedha nchini Kenya, inasema licha ya makadirio ya bajeti hii kuwasilishwa mapema, yataanza kutekelezwa mwezi wa kifedha wa Juni.

Mamlaka ya mapato nchini Kenya KRA, imepewa jukumu la kukusanya Shilingi Trilioni 1.9 kupitia utozwaji kodi.

Serikali nayo italazimika kutafuta Shilingi Bilioni 900 kufanikisha miradi mbalimbali.

Sekta zinazopewa nafasi kubwa katika bajeti hii ni pamoja na usalama, afya, elimu na miundo mbinu kama barabara.

Wizara ya fedha imesema pia kuwa kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kufanikisha mradi wa kuanza kuchimba mafuta na kujenga bomba la kusafirisha.

Wakenya wamekuwa na hofu kuwa huenda hatua ya serikali kukopa fedha nyingi kwa sababu mbalimbali huenda kukaifanya serikali kuongeza kodi lakini Wizara ya fedha imesema haitafanya hivyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.