Pata taarifa kuu
TANZANIA

Baada ya kusota rumande Serikali yaagiza Polisi kumuachia msanii Ney Wa Mitego

Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo nchini Tanzania, Harrison Mwakyembe ameliomba jeshi la polisi nchini humo, kumuachia msanii wa Bongofleva Emmanuel Elibariki maarufu kama “Nay wa Mitego” aliyekuwa anashikiliwa kwa tuhuma za kutoa wimbo usio na maadili “WAPO”.

Msanii Emmanuel Elibariki  maarufu kama Ney Wa Mitego
Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney Wa Mitego YouTube/Shot/
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mjini Dodoma, waziri Mwakyembe amesema kuwa aliwasiliana na rais Magufuli ambaye alimuelekeza kuwa wimbo huo haukuwa na shida yoyote ya kimaadili na kwamba hata yeye binafsi ameupenda na anamtaka msanii huyo aongeze baadhi ya maneni kwenye wimbo wake.

“Kwakweli ule wimbo ni mzuri hata muheshimiwa rais amesema anaupenda na kusema ukweli ile biti imetulia,” amesema waziri Mwakyembe wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na wimbo huo.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa raia Magufuli hata amependekeza kwenye wimbo wake aongezek kama maneno “hata wakwepa kodi...wapoo’! Ili kuufanya unoge zaidi kutokana na ujumbe wake kuwa ulilenga kuiamsha jamii juu ya athari za utawala mbaya na rushwa kwenye jamii.

“Nimechukua hatua kama waziri mwenye dhamana kuwaomba polisi kumuachia huyo kijana, wamuache kumuhoji na hata nitafurahi nikimuona kesho akija Dodoma ili nimshauri nini cha kufanya kwenye wimbo wake ili uwe mzuri zaidi,” alisema waziri Mwakyembe.

Sikiliza wimbo wa Ney Wa Mitego uliokuwa umezuiwa na Baraza la Sanaa Tanzania.

03:44

Wimbo wa Msanii Ney wa Mitego WAPO ambao sasa umeruhusiwa kutumika

Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa wao kama Serikali na wizara hawaoni madhara ya wimbo huo lakini akataka uboreshwe zaidi na kuwataja watu kama wakwepa kodi na wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Kabla ya uamuzi huu wa waziri Mwakyembe, hata baraza la sanaa nchini humo lilikuwa tayari limetoa taarifa kwa vyombo vya habari ikitangaza kuupiga marufuku wimbo huo kutokana na kile baraza hilo lilisema ni wimbo wake kukosa maadili na kutumia lugha ambayo haikuwa na staha.

Msanii Ney wa Mitego alikamatwa juzi usiku mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam kwa mahojiano na polisi kuhusiana na mashari yaliyokuwa kwenye wimbo wake.

Tayari mijadala mizito imeibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uamuzi wa Basata na huu wa sasa unaoteolewa na wizara kuhusu kuachiwa huru kwa msanii huyo.

Wadadi wa mambo wanahoji kuhusu hatau za harakaharaka zilizochukuliwa na vyombo vya dola nchini Tanzania na baadae baraza la sanaa kutangaza kuufungia wimbo huo ambao sasa wizara inasema wimbo haukuwa na shida na hata rais mwenyewe anaupenda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.