Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAUAJi-USALAMA

Visa vya mauaji vyaongezeka nchini Burundi

Nchini Burundi, mwili wa afisa wa ngazi ya juu katika polisi, uligunduliwa Jumatatu asubuhi Machi 20 katika majengo ya Parokia ya Kanisa Katoliki mjini Bujumbura, wakati mwili mwingine uligunduliwa Jumatatu wiki hii katika mkoa jirani wa Muramvya.

Polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Aprili 12, 2016.
Polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Aprili 12, 2016. STRINGER / cds / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi amehakikisha kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uchunguzi unaendelea, wakati ambapo moja ya mashirika makuu yanayotetea haki za binadamu nchini Burundi, Ligue Iteka, lililopigwa marufuku tangu mwanzoni mwa mwaka huu, limebaini kwamba machafuko na visa vya mauaji vimeongezeka nchini humo, huku likisema ukandamizaji huo unaendeshwa na vikosi vya usalama vinavyounga mkono utawala wa Pierre Nkurunziza, vikosi ambavyo vinaoongozwa kwa idadi kubwa na kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD.

Miili ya watu waliouawa kikatili imeendelea kugunduliwa sehemu mbalimbali nchini Burundi.

Kwa mujibu wa shirika la Ligue Iteka, miili 22 ya watu waliouawa iligunduliwa katika mitaa au misitu kuanzia Januari, 17 hadi Februari 24 na tayari miili 24 imegunduliwa ndani ya kipindi cha wiki tatu za mwezi huu wa Machi.

Shirika hili kongwe la haki za binadamu nchini Burundi, limeinyooshea kidole cha lawama serikali ya Burundi inayoongozwa na chama kutoka kundi la zamani la waasi wa Kihutu la CNDD-FDD kuhusika na mauaji hayo.

"Mara nyingi, miili hii ya watu waliouawa haitambuliwi.Hali hii inatutia wasiwasi mkubwa, na ndio maana kila wiki tunailalamikia kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati. "

Makamu wa kwanza wa rais nchi Burundi, Gaston Sindimwo amekosa tuhuma hizo, huku akihakikisha kwamba "usalama umeimarika,".

Kuhusu ombi la uchunguzi huru, gaston Sindimwo hataki kusikia hilo, akibaini kwamba Burundi ina wachunguzi wazuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.