Pata taarifa kuu
EAC

Wabunge EAC waonya kuvunjika kwa Jumuiya ikiwa viongozi hawachangii bajeti

Bunge la afrika mashariki limeweka wazi, suala la kuzorota kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika utoaji michango ambapo wameonya kuwa ikiwa hatua hazitachukuliwa haraka jumuiya hiyo itaelekea pabaya. 

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipokutana wakati mmoja jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipokutana wakati mmoja jijini Dar es Salaam. eac photo hand out
Matangazo ya kibiashara

Kutotekelezwa kwa mirandi mbalimbali ya kimaendeleo, kutolipwa mshahara kwa wafanyakazi kwa mda ni baadhii ya changamoto zilizo anza kujitokeza kutokana na nchi hizo kutochangia kwa wakati.

Wabunge hao wamesema ingawa kumebaki miezi kadhaa ili mwaka wa fedha utamatike, mchango uliotolewa haufikii hata nusu ya bajeti iliyotolewa na hilo ndio limewafanya wabunge hao kuomba serikali za nchi wanachama kutoa maelezo na kutekeleza swala la utoaji wa michango kwani changamoto zinazidi kuongezeka.

Aidha licha ya mengi yaliyozungumzwa pia wabunge hao wamewaagiza mawaziri wa jumuhi hiyo kujadili kwa haraka na ma raisi .

Kwa upande wao mawaziri ambao pia wameudhuria vikao vya bunge wametangaza kwamba suala hilo linaenda kupewa uzito na muda si mrefu litajadiliwa na viongozi wa nchi.

Wabunge hao wamesema serikali zinapaswa kujihadhari ili Jumuiya isije kuvunjika tena.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.