Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-AFYA

Madaktari kuachishwa kazi nchini Kenya

Hospitali za Kenya zimeanza kuwafukuza madaktari walio katika mgomo kwa miezi mitatu sasa wakidai kuongezwa mshahara na kuboresha hali ya maisha.

Madaktari walio katika mgomo nchini Kenya wanomba nyongeza ya mshahara ya 50% kama ilivyokubaliwa katika mkataba uliosainiwa mwaka 2013.
Madaktari walio katika mgomo nchini Kenya wanomba nyongeza ya mshahara ya 50% kama ilivyokubaliwa katika mkataba uliosainiwa mwaka 2013. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kutopatiwa suluhu yoyote katika mazungumzo na madaktari wa Kenya walio katika mgomo, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa maneneo makali Jumanne wiki hii akiwashambulia madaktari takriban 5,000 madaktari wa hospitali za umma.

Kufuatia kuzorota kwa shughuli katika vituo vya afya vya umma, serikali imetishia kuajiri madaktari kutoka Cuba watakaochukua nafasi za madaktari wanaoendelea na mgomo.

Madaktari walio katika mgomo nchini Kenya wanomba nyongeza ya mshahara ya 50% kama ilivyokubaliwa katika mkataba uliosainiwa mwaka 2013, lakini makubaliano hayo hayajatekelezwa. Mpaka sas serikali imekua ikipendekeza nyongeza ya mshahara ya 40%.

Madaktari walio katika mgomo pia wanalalamikia rushwa ambayo imekithiri nchini Kenya na wanaomba marupurupu ya ziada kwa hospitali za umma.

Inaarifiwa kwamba chama cha madaktari kimesaini hati ya kumaliza mgomo na wameiomba serikali kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.